waziri wa mambo ya ndani Mathias Chikawe Akizungumza na waandishi wa habari wa BBC
Serikali ya Tanzania imeunda kikosi maalumu kwa ajili ya kupambana na vitendo vya ukatili wanaofanyiwa watu wenye ulemavu wa ngozi –Albino- na huku ikitangaza pia kupiga marufuku kuanzia leo wapiga ramli wote ambao wanaelezwa kuchangia mauaji ya watu hao.
Waziri wa Mambo ya Ndani
Mathias Chikawe Ameitaja mikoa inayotarajiwa kuanza kwa operesheni
maalum ya kupambana na vitendo vya ukatili dhidi ya walemavu katika
juhudi za kukomesha kabisa matukio hayo, ambayo yameelezwa kuanza
kuibuka tena.
Mikoa hiyo ni Mwanza, Simiyu, Geita, Tabora na
Shinyanga.Operesheni hiyo pia inatarajiwa kuendelea katika mikoa
mingine.Aidha amesema operesheni hiyo itaanza baada ya wiki mbili kwa
ushirikiano wa polisi na wawakilishi kutopka chama cha watu wenye
ulemavu Tanzania.
Kazi ya kikosi hicho ni pamoja na kupitia pia
kesi zote zilizowahi kufikishwa mahakamani kuhusiana na vitendo
hivyo.kizungumzia kuhusiana na kupigwa marufuku kwa wapiga ramli nchi
nzima, Waziri Chikawe amesema jeshi la polisi litaandaa operesheni
maalum kuwatafuta na kuwashtaki.
Amesema wapiga ramli hao wanajulikana na wananchi wanaomba kusaidia kuwatambua.
Aidha
amewataka wananchi kutoa ushirikiano katika kufanikisha zoezi hilo
zima, ikiwemo pia kuyataka madhehebu ya dini mbalimbali na mashirika ya
kijamii kutoa elimu juu ya jambo hilo.Sababu kubwa iliyotajwa
inayosababisha watu kutafuta viungo hivyo vya binadamu inaelezwa kuwa ni
kupata utajiri.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment