January 26, 2015

 
 Kamanda wa UVCCM mkoa wa Dar es salaam Mh. Abbasi Mtemvu.
Umoja wa vijana CCM mkoa wa Dar es Salaam- UVCCM umetoa tamko kwa serikali kuwa watahakikisha wanafanya maandamano ya amani yatakayo shirikisha Wamachinga, Bodaboda na Mamalishe ili kuishinikiza serikali inayo ongozwa na chama chao ku
Wakizungumza mbele ya Mbunge wa Kwahani na Waziri wa ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi kabla ya kumsimika Kamanda wa UVCCM mkoa wa Dar es salaam Mh. Abbasi Mtemvu kwa niaba ya katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, Viongozi wa UVCCM mkoa wa Dar es salaam wamesema kuwa pamoja na vijana wengi kukosa ajira na wengi kuingia katika ajira zisizo rasmi ikiwemo bodaboda na ujasiriamali lakini serikali ya chama cha mapinduzi imekuwa ikiwanyanyasa ikiwemo kuwapora mali zao na kugawana bila sababu za msingi.
Akihutubia wafuasi wa chama hicho waliojitokeza kwa wingi katika viwanja vya Mwembe Yanga Mh. Mwinyi amehaidi kuyafikisha malalamiko hayo sehemu husika ili yafanyiwe kazi ambapo pia ametoa wito kwa jamii kuhakikisha kuwa wanadumisha amani na utulivu na kuepukana na makundi yasiyo litakia taifa mema hususani katika kipindi ambacho nchi inaelekea katika uchaguzi mkuu.
Akizungumza mara baada ya kusimikwa ukamanda huo Mh. Mtemvu ameahidi kusimama kidete katika kuyashughulikia matatizo ya vijana hususani katika sekta ya upatikanaji wa mikopo yenye riba nafuu ambayo ana imani itawasaidia vijana kujikwamua kiuchumi.
acha unyanyasaji 

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE