Wafugaji jamii
ya wamasai na wabarabaigi mkoani Morogoro wamefunga minada yote ya
kuuza mifugo mkoani Morogoro kwa muda usiojulikana wakilalamikia
serikali kushindwa kukomesha vitendo vya uonevu wanavyofanyiwa na
madereva wa bodaboda kwa kupigwa na kufukuzwa kila wanapongia katika
mji wa morogoro.
Wakizungumza kwenye mkutano uliojumuisha wafugaji kutoka wilaya za Morogoro, Gairo Mvomero na Kilosa wakiwa na viongozi wao wakuu wa jadi wanaofahamika kama malaigwenani wafugaji hao wameazimia kufunga minada yote kwa muda usiojulikana.
Mbali na maamuzi hayo wafugaji hao pia wameazimia kuacha kuuza maziwa na mifugo mkoani Morogoro na watakaobainika kukiuka agizo hilo watalipishwa faini ya shilingi milioni moja hadi hapo serikali itapoamua kuingilia kati migogoro ya wakulima na wafugaji.
Katika hatua nyingine kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Morogoro imetembelea kijiji cha Mabwegele kujionea athari za watu kuchomewa nyumba ambapo mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt Rajab Rutengwe amesema serikali haitasita kuchukua hatua kwa waliohusika na tukio hilo, na tayari wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi imemteua Bw Paul Kimiti kufika mkoani hapa kufanya usuluhishi kwa lengo la kumaliza migogoro hiyo.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment