Nimeongea Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Prof. John Nkoma, kumuagiza azungumze
na makampuni ya simu juu ya mabadiliko ya bei za bundles: ukubwa,
ughafla na upamoja (mitandao yote). Nimewaagiza pia watoe majibu kwa
umma haraka iwezekanavyo. Makampuni ya simu hayapaswi kupanga au
kuratibu kwa pamoja bei; tukigundua hilo limetokea ni ukiukwaji wa
kanuni za ushindani wa soko. Sheria ya udhibiti wa Mawasiliano haitupi
nguvu (Serikali) ya kupanga bei,
isipokuwa interconnection fees. Inawezekana gharama za uendeshaji,
ikiwemo umeme, zinapanda, lakini hakuna kodi mpya ya Serikali tangu
baada ya bajeti. Huko nyuma ushindani ulishusha bei kwasababu hakukuwa
na bei elekezi. Bado niko nje ya nchi kwa safari ya Kiserikali, lakini
nimekuwa nalifuatilia suala hili kwa karibu. Pia nimeongea na Mkurugenzi
Mkuu wa Vodacom, Rene Meza, kuhusu suala hili leo (jana)
asubuhi.......... KUTOKA kwenye page yake ya instagram..
0 MAONI YAKO:
Post a Comment