Uongozi wa muziki nchini marekani unao muongoza msanii wa R&B Chris
Brown umetoa taarifa kwa uongozi wa muziki Tanzania unao muongoza msanii
kutoka Tanzania ALI KIBA msanii ambae yupo chini ya uongozi wa Kampuni
za SAMSUNG. Kwa taarifa zilizopo katika mtandao wa VIP Beats nchini
marekani zinaeleza kua tarehe 24 mwezi wa 11 mwaka 2014 uongozi wa
msanii Chris Brown ulipokea maombi ya muungano wa wasanii wawili kufanya
wimbo wa pamoja kati ya msanii Ali kiba na Chris Brown maombi hayo
yaliambatanishwa na Softcopy zilizobeba nyimbo tatu za msanii Ali kiba
ikiwemo SINGLE BOY, MWANA pamoja na wimbo aliofanya katika project ya
ONE 8.
Uongozi wa Chris Brown umethibitisha kupokea taarifa za maombi hayo na
umeonesha kupenda sauti ya msanii Ali kiba na kutoa tamko kua wapo
tayari kusimamia kazi ya pamoja itakayofanywa na wasanii hawa. Upande wa
msanii Chris Brown amesema hana tatizo yupo tayari kushirikiana na
msanii Ali kiba kwani alipata nafasi ya kutazama project ya One 8 na
ameona kiwango cha msanii Ali kiba kinaridhisha japokua anahitaji
marekebisho madogo sana. BBC SWAHILI Tunampongeza msanii Ali kiba kwa
juhudi zake tunamtakia kila lakheri katika kazi hii, kuipata habari hii
kamili tembelea mtandao wa VIP Beats, Channel 0 au unaweza kuipata
katika American Spring news.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment