February 03, 2015

 
 Siku ya jana Th 2 Febr 2015, tasnia ya burudani ilipata pigo baada ya bondia francis cheka kuhukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela na fidia ya Shilingi milioni moja kufuatia kesi iliyokuwa ikimkabili ya kumpiga Mfanya kazi wake wa Bar (meneja wake)
  
mbalimbali wametoa mitazamo yao juu ya hukumu hiyo

Saddiq Rajabu Ninachoamini kaka mkubwa alipata hasira na kumpiga meneja wake baada ya dhulma aliyohisi imeletwa na meneja huyo ni hulka ya binam hatupendi kudhulumiwa.
Si jambo jema alilotenda kuchukua sheria mkononi lakini naamini kulikua na nafasi ya hawa watu wawili wangewekwa chini na kulimaliza jambo lao kwa njia ya amani kama ilivyo desturi yetu sisi waungwana tumeyaona mengi ya hivyo katika jamii yetu.
Nadhani kuna ubabe fulani wa kukomeshana umejitokeza hapo baina yao tena nashawishika hata kuamini kuna mikono ya watu wengine imetumika kuchochea, tunajijua sisi wabongo kwa visasi visivyo na maana
Mwisho pia naamini kukosa kwa Bondia Francis cheka kuwa na menejimenti nzuri ambayo ingeweza kulisimamia hilo swala kwa umakini mzuri.yasingetokea haya tuliyoyasikia jana.
 
Adella Tillya
Adella Tillya Siku yangu leo haikuwa poa sana kutokana kupata taarifa juu ya kilichompata my best bro Francis Cheka na nilipata bahati za kuzungumza nae kwa njia ya simu akiwa mahakamani kwa kweli imenishtua na kunihuzunisha pole sana my kaka hope tuko pamoja hizo zote ni changamoto za maisha ila tuko wote bega kwa bega watu wangu wa Moro na wapenzi wa Cheka tuendelee kushirikiana nae na pole kwa wote. No one is perfect. 
Nickson Mkilanya
Nickson Mkilanya Bondia francis cheka kahukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kwa kosa la kufanya shambulio ktk mwili dhidi ya mfanyabiashara wa eneo la mafiga ktk manispaa ya morogoro. Lkini nikizungumza na cheka baada ya hukumu hiyo anasisitiza kuwa hakumpiga mfanyabiashara huyo akidai kuwa alikuwa akimdai fedha zake zilizotokana na biashara ya bar aliyokuwa amemkabidhi kuiendesha ktk eneo la sabasaba ktk manispaa ya morogoro. Aidha amesema anajua kuwa kufungwa kwake kuna shinikizo kutokana na kupinga dhulma dhidi yake. Duh roho imeniuma saana ntajua namna ya kumsaidia
Asalam alekh

Unaweza kutoa mitazamo yako juu ya hukimu hiyo

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE