
Mitandao ya kijamii imetusogeza karibu, Facebook ni moja ya mitandao hiyo, lakini kurasa za mtumiaji wa mtandao kama Facebook huwa zinaendelea kuwepo hata kama ikitokea mtumiaji amefariki.
Facebook wameenda
mbali zaidi, muda si mrefu kutakuwa na setting ambayo mtumiaji wa
mtandao huo anaweza kuamua kama ukurasa wake huo ufutike au uendelee
kuwepo huku ukiendeshwa na mtu mwingine, au ubaki kwa ajili ya
kumbukumbu za mtumiaji kama ikitokea mtumiaji amefariki.
Hii itaanza kufanya kazi hivi karibuni
Marekani na baadaye wataalam wa Facebook wanaangalia namna ya kila
mtumiaji kuweza kuufanya hivyo ukurasa wake wa Facebook
0 MAONI YAKO:
Post a Comment