February 10, 2015

Mahakama ya Malaysia imekataa kubadilisha uamuzi dhidi ya kiongozi wa Upinzani Anwar Ibrahim   
Mahakama ya juu zaidi nchini Malaysia imekataa kubadilisha uamuzi kuhusu kesi ya kulawiti inayomkabili kiongozi wa upinzani Anwar Ibrahim.
Baadhi ya wanasiasa wa Malysia, watetezi wa haki za kibinadam pamoja na Bwana Anwar mwenyewe, wanaamini kuwa hukumu hiyo ni mbinu tu ya wapinzani wake kutaka kumhujumu kisiasa.
Anwar ambaye zamani alikuwa naibu waziri mkuu, alikihama chama tawala na kujiunga na upinzani.
Licha ya hayo yote, mkewe, Wan Azizah Wan Ismail, anasema kuwa mumewe hatakoma kupigania maisha ya watu wa nchi hiyo:
Bwana Anwar alikata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama uliokuwa umetolewa mwezi machi mwaka uliopita kwa kumlawiti msaidizi wake wa kiume mwaka 2008.
  
 Mapenzi ya jinsia moja ni haramu nchini Malaysia.
Bwana Anwar anasema kuwa hiyo ni sehemu ya kampeni ya chama tawala ya kumchafulia jina.
Anakabiliwa na kifungo cha hadi miaka mitano gerezani lakini anasema ana hofu kuwa serikali huenda ikaongeza miaka ikiwa atashindwa kwenye rufaa hiyo.
Baadhi ya wanasiasa wa Malysia, watetezi wa haki za kibinadam pamoja na Bwana Anwar mwenyewe, wanaamini kuwa hukumu hiyo ni mbinu tu ya wapinzani wake kutaka kumhujumu kisiasa.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE