Mlinzi wa timu ya Liverpool Kolo
Toure ameuthibitishia ulimwengu kuwa anastaafu kusakata kabumbu la
kimataifa akiwa na timu ya nyumbani Ivory Coast,wiki moja baada ya
kuwasaidia Tembo hao kutwaa kombe la mataifa ya Afrika .
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka thelathini na tatu sasa, ameeleza wazi kuwa
mchezo wake wa mwisho ni dhidi ya timu ya Equatorial Guinea hapo ndo
mwisho wake kuonekana viwanjani.
Kolo anasema anaipenda nchi yake
na hasa anachokipenda zaidi maishani mwake ni Kandanda,lakini
akatanabaisha hufika wakati asitishe.
Kolo ameyasema hayo
alipokuwa akizungumza na chombo kimoja mjini Abidjan, Toure anasema
najisikia vibaya sana kuwafahamisha kuwa niwakati wangu kuwaaga. Lengo0
langu lilikuwa kushinda katika michuano ya kombe la mataifa ya Africa,
na nakubali ulikuwa ni uamuzi mgumu sana kuufanya.
Toure amekuwa
kiungo muhimu sana katika kuutengeneza ushindi wa timu na taifa lake
katika kipindi cha miaka ya 2006, 2010 and 2014 akiwa na kikosi cha timu
yake ya taifa katika michuano ya kombe la dunia..
Ametua katika
michuano ya kombe la mataifa ya Afrika mara saba ,akiwa amekosa penati
mbili katika mechi mbili za fainali dhidi ya Egypt mwaka 2006 na ingine
ni ile ya Zambia mwaka 2012 kama unakumbuka vyema.
Na kolo amemtaja mrithi wake kuwa ni Ousmane Viera Diarrassouba, ambaye atakaba nafasi ya ulinzi baada yake.
Nadai huwa hafanyi makosa pindi afanyapo uchaguzi wa nani akae wapi, naamini mrithi wangu atawapika vyema vijana wawili Eric Bailly na Wilfried Kanon.na hivyo anaamini Viera atamuwakilisha vyema.
Kolo alianza kuonesha cheche zake katika timu ya ASEC Mimosas ya Abidjan, Toure kisha akaelekeza daluga zake kwenye timu ya Arsenal mnamo mwaka 2002 na alikuwa chachu ya kutofungwa kwa msimu wa miaka miwili mfululizo nazungumzia miaka ya 2003/4.
Lakini baadaye alimwaga wino katika kilabu cha Manchester City mnamo mwaka 2009 kabla hajaelekea katika timu ya Liverpool kwa uhamisho wa bure msimu uliopita.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment