Mtu aliyezuiliwa kuingia Paris Metro train na mashabiki wa timu ya mpira ya Chelsea kwa sababu ya ubaguzi wa rangi ametaka waadhibiwe.
Mtu huyo mwenye miaka 33 anayeitwa Souleymane S aliambia gazeti la Le Parisien: “Hawa watu, hawa mashabiki wanapaswa kufungwa".
Video ilionyesha mtu huyo akizuiliwa kuingia kwenye Metro na akisukumwa na mashabiki hao.
Watu walisikika wakiimba: "Sisi ni wabaguzi wa rangi na hivyo ndivyo tupendavyo".
Kanda hiyo ya video ilitolewa na gazeti la the Guardian lililotoa ripoti kuwa tokeo hilo lilifanyika Richelieu-Drouot katika mji mkuu wa Fance siku ya Jumanne kabla mechi ya Champions Legue.
TPDC YANG'ARA KATIKA MAONESHO YA 49 YA SABASABA, YASHINDA TUZO YA MAZINGIRA
-
SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limeibuka mshindi katika
Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, maarufu kama
Sabasaba,...
6 hours ago
0 MAONI YAKO:
Post a Comment