Amboni Tanga: Askari Polisi wapambana na majambazi wenye silaha za moto
Tanga kumenuka, magaidi wenye silaha nzito wanapambana na askari polisi muda huu. Askali wa jeshi la wananchi wameingilia kati na silaha za kisasa. Sasa hivi wanaelekea kwenye mapango ya Amboni.Askari wote wameshatawanyika eneo la Tukio na walichokuta ni Pikipiki, baiskeli, vyakula na nguo.
UPDATES:
Yapata wiki moja Polisi walimkamata mtuhumiwa mmoja anajulikana kwa jina la Master ambae inasemekana ndiye aliyekuwa akiratibu uporaji wa silaha vituo vya polisi na polisi wenyewe. Matukio haya yametokea kule Ikwiriri Rufiji Pwani baada ya kituo kuvamiwa na Tanga Chumbageni kwa askari kuporwa silaha wakiwa katika doria.
Katika kutumia weledi wao wa kupata habari, ililazimika sasa polisi waende eneo ambalo mtuhumiwa anasema ndiko silaha wanazopora zilipofichwa. Alieleza silaha wanaficha maeneo ya Amboni ambako Wachina waliojenga barabara ya Horohoro waliweka kambi. Kwa hiyo magaidi hayo hayapo mapango ya Amboni tunayoyafahamu.
Baada ya kufika eneo la tukio mtuhumiwa akiwa na pingu alijirusha kwenye pango hilo huku polisi wakiwa wanashangaa nini kimetokea. Ikumbukwe mtuhumiwa huyo alikuwa na pingu. Baada ya mtuhumiwa tu kutua chini au kiliposikika kishindo basi haikupita muda mvua ya risasi ilianza kunyesha kuelekea polisi walipo pamoja na mabomu ya kurusha kwa mikono. Bomu mojawapo lilifanikiwa kumjeruhi askari polisi mmoja ambaye ameshonwa nyuzi kama kumi na moja hivi. Kwa hiyo hakuna polisi aliyekufa kwenye tukio hilo.
Baada ya kuona hali imekuwa ngumu ilibidi OCD aliyekwenda kwenye tukio kuomba msaada zaidi kwa FFU Tanga. Napo hali ikawa tete, ndipo ilipolazimu kuomba msaada kutoja Jeshi la Wananchi Tanzania.
Kama uelewevyo kuomba Jeshi la Wananchi kuingilia kati na lazima CDF atoe kibali na ithibitike kuna ulazima.
Hatimaye saa tisa za mchana kibali kilipataka na Jeshi la Wananchi kwenda eneo la tukio. Walipofika waliona kuna ulazima wa kutumia silaha nzito ili kulifumua pango hilo ambalo ili kujua kilichopo. Kuanzia hapo mizinga imekuwa ikisikika maeneo hayo ishara ya kwamba wanaume wapo kazini.
Katika kuongeza nguvu kikosi maalumu kimeongezwa kutoka Dar ili kuhakikisha hali inakuwa salama.
Hadi leo asubuhi bado mizinga ilikuwa ikisikika licha ya kwamba saizi haisikiki tena.
Lengo la hao Al Shabab inasadikiwa ni kutoka kuwakomboa wenzao ambao wamefungwa au wapo Magerezani. Kwa mantiki hiyo, sakata kubwa lipo katika ulinzi wa Magereza ambapo wanasema ni wakati wa kulipa kisasi makubwa ambayo waliyataja ni Gereza Lilungu lililopo Mtwara, Gereza Arusha na Gereza Segerea lililopo Dar.
Pamoja na hayo bado ukweli unabaki wazi wanaweza kuvamia gereza lolote ili kutimiza malengo yao.
Ni jukumu sasa la vyombo vyetu vya ulinzi na Usalama kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuhakikisha hali haiwi alijojo.
Mungu Ibariki Tanzania.
Chanzo Jamiiforums
0 MAONI YAKO:
Post a Comment