February 11, 2015

UN kutoisaidia Kongo DR kupambana na FDLR  
 Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kimesitisha uungaji mkono wake kwa vikosi vya Kongo kwa ajili ya kuendesha oparesheni dhidi ya waasi wa Kihutu wa Rwanda wa FDLR, kufuatia tuhuma dhidi ya majenerali wawili wa Kongo za kukiuka haki za binadamu. Kikosi cha kulinda amani nchini Kongo DR kimebainisha masikitiko yake kufuatia kuhusishwa majenerali wawili wa jeshi la Kongo (FARDC) na ukiukaji wa haki za binadamu na kwa hiyo kikosi hicho kimeamua kusimamisha msaada wake kwa jeshi hilo dhidi ya oparesheni za kuwafurusha waasi wa Rwanda wa FDLR. Waasi wa FDLR wanawajumuisha wanajeshi wa zamani wa Rwanda na wanamgambo wa Kihutu waliohusika na mauaji ya kimbari nchini humo ya mwaka 1994, waasi ambao kwa miaka kadhaa sasa wamekuwa wakisababisha machafuko katika eneo la Maziwa Makuu la katikati mwa Afrika.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE