March 28, 2015

 Baadhi ya wasanii waliopo chini ya Fantastic
 Kampuni mpya ya Fantastic & Cool Object ya nchini Tanzania, imedhamilia kuleta mabadiliko kwa watanzania kwa kuanzia na wasanii wa Bongo Fleva.

 Mkurugenzi wa Fantastic & Cool Object bw. Kris Mutsmamoyo
 Akizungumza na ubalozini.blogspot.com Meneja wa Kampuni hiyo ndugu  Constantine Mihambo, amesema lengo na dhamira kubwa ya Kampuni hiyo ya kisasa ni kusaidia jamii iliyokata tamaa na kuwapa tumaini jipya la kimaisha kwa kuwasaidia wajikwamue kiuchumi na kufikia malengo ikiwemo  kuzisambaza kazi zao ndani na nje ya Tamnzania na kuwafanya wasanii kuwa wa kimataifa
Meneja Constantine Mihambo
 Mihambo amesema katika kuhakikisha hilo, tayari wameshaanza na baadhi ya wasanii na kufanya nao Project ya wimbo wa Rais Kikwete ambao umeshaanza kufanya vizuri.
  "Tumeonelea tuanze na wimbo wa kikwete ambao tumetafakali na kuuona mchango mkubwa sana wa Raisi huy anayemaliza muda wake,  kwa kulitambua hilo tumetunga wimbo huo ambao tayari umeanza kufanya vizuri na kwa sasa tayari tumeanza kufanya Video ya wimbo huo chini ya DR. Jazzy Wizzy wa Priceless ambaye tunaamini anafanya kazi nzuri"

  Mihambo amesema Video ya wimbo huo inafanyika Morogoro,Dodoma,Bagamoyo, Kilimanjaro na Zanzibar.

Baadhi ya wasanii walipo chini ya Kampuni hiyo ni pamoja na Ainea,Halice, Man Ngingo na Krisi mwenyewe.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE