March 26, 2015

 
 Kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachoshughulikia mihadarati na Uhalifu kimesema kuwa maharamia wameteka meli mbili za Iran za kuvua samaki katika ufuo wa Somalia.
Utakeji huo ni wa kwanza kufaulu tangu mwaka 2012.
Ushikaji doria na matumizi ya walinzi wenye silaha umesaidia kupunguza uharamia katika ufuo wa Somalia, ambao awali ulikuwa ukishirikisha zaidi ya meli 200 kwa mwaka.
Umoja wa Mataifa unasema kuwa wafanyakazi 48 wametekwa nyara katika uharamia huo.
Taarifa hiyo inasema kuwa meli hizo, zilizokuwa zikivua samaki bila kibali katika fuo hizo za Somalia zimepelekwa katika kijiji cha Pwani cha El Huur katikati mwa Somalia.
Ingawa uharamia ulikuwa umepunguka, idadi ya wavuvi haramu imeongezeka.
Uvuvi haramu ndio ulioanzisha mtindo wa kuteka meli Somalia.
Umoja wa Mataifa umeonya kuwa iwapo meli za kigeni zitaendelea kuvua samaki kimagendo katika ufuo wa Somalia, visa vya uharamia navyo vitaongezeka.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE