
Wakristu wazika wapendwa wao waliouawa katika milipuko makanisani
Waumini wa dini ya kikristu nchini
Pakistan wamekusanyika kwa maziko ya waathiriwa wa mauaji ya siku ya
jumapili yanayoaminiwa kufanywa na wanamgambo wa Taliban.
Maelfu ya wanajeshi walizingira eneo linaloaminiwa kuwa na wakristu wengi zaidi jijini Lahore wakati wa maziko hayo.Huku kukiwa na hali ya wasiwasi na ulinzi mkali familia katika mji wa Yohnanabad waliwazika wapendwa wao

Jamaa ya wale waliouawa wakiomboleza
Mahali hapo pali zingirwa na
walinda usalama na kila mmoja aliyekuwa akiingia mahali pale kuhudhuria
mazishi hayo alikuwa anapekuliwa .Siku ya jumatatu walinda usalama walilazimika kuwatawanya waandamanaji kwakutumia mizinga ya maji .
Waandamanaji hao wamekuwa wakipinga mashambulizi dhidi ya wakristu yaliasababisha vifo vya watu 17.
Muda mfupi baada ya mlipuko, raia wenye hasira waliwavamia watu wawili na kuwapiga hadi kuwauwa.

Waandamanaji wakikristu walikabiliana na polisi wakipinga mauaji katika makanisa
Waziri wa mambo ya ndani wa
Pakistan ametaja kuwawa kwa watu hao wawili na kitendo ya kupigwa kanisa
kwa bomu kama vitendo vya kigaidi.Jamii ya wakristu wanasema maadamano hayo ni ishara yao ya kuonyesha kuwchoshwqa na serikali ambayo wanahisi imewasahau.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment