April 04, 2015

Kundi la wanamgambo wa al-Shabab wa Somalia limetishia kuishambulia tena Kenya na kusisitiza kwamba, Wakenya watakabaliwa na vita vya muda mrefu na vya kutisha. Taarifa ya wanamgambo wa al-Shabab imebainisha kwamba, muda sio mrefu Kenya itakabiliwa na mashambulio mengine ya wanachama wake. Kenya imeingia katika vita vya muda mrefu na vya kutisha na al-Shabab, imebainisha taarifa ya wanamgambo. Taarifa hiyo ya wanamgambo wa al-Shabab imebainisha kuwa, watu ambao wanashiriki katika uchaguzi na kuziunga mkono sera za serikali ya Kenya wanapaswa kulipa gharama ya hayo kwa damu zao. Sehemu nyingine ya taarifa hiyo imetanabahisha kwamba, mashambulio ya al- Shabab yatawalenga raia wa Kenya katika shule, vyuo vikuu na hata majumbani mwao kutokana na hatua yao ya kuiunga mkono serikali ya nchi hiyo ambayo imetuma majeshi yake Somalia kwa ajili ya kupambana na wanamgambo wa al-Shabab. Vitisho vya kundi la kigaidi la al-Shabab vimetolewa siku mbili tu baada ya Chuo Kikuu cha Garissa huko Kenya kushambuliwa na wanamgambo wa kundi hilo ambapo watu karibu 150 waliuawa. Wakati huo huo, serikali ya Kenya imetangaza kuwa, watu watano wametiwa mbaroni wakihusishwa na shambulizi la siku ya Alkhamisi. Katika upande mwingine, serikali ya Kenya imetangaza kuwa, taifa hilo halitasalimu amri mbele ya ugaidi na kwamba, litaendelea kupambana nao kwa nguvu zake zote.

Chanzo: Idhaa ya Kiswahili ya Iran

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE