April 26, 2015

Filamu ya Sniper yapigwa marufuku Maryland  
Wanachuo wa Kiislamu wa Chuo Kikuu cha Maryland nchini Marekani wamepongeza na kukaribisha hatua ya kufutwa uamuzi wa kuoneshwa filamu ya American Sniper.
Wanafunzi hao wamesema hiyo ni hatua nzuri ya kujenga mazingira ya amani na ya kiadilifu katika chuo hicho. Uamuzi huo ulichukuliwa baada ya malalamiko ya wanafunzi Waislamu wa Chuo Kikuu cha Maryland. Wanafunzi hao wanasisitiza kuwa filamu hiyo inavunjia heshima Uislamu na Waislamu na kueneza hisia za kuhujumu na kupiga vita Uislamu. Taarifa iliyotolea na jumuiya ya Wanafunzi Waislamu wa Chuo Kikuu cha Maryland imesema: Filamu hiyo inawadhihirisha Waislamu kuwa ni hawana utu au kwamba ni watu wasiostaarabika na kueneza fikra ya mauaji ya umati. Imesisitzia kuwa filamu ya ya American Sniper inawavunjia heshima na kuwadunisha Waislamu kote duniani.
Waislamu katika vyuo vikuu vingine vya Marekani pia wametaka kusimamishwa zoezi la kuoneshwa filamu hiyo na wamekuwa wakitumia nyenzo mbalimbali kueleza malalamiko yao.
Filamu iliyotengenezwa Marekani ya American Sniper inaeleza kisa cha Chris Kyle askari wa Marekani aliyetumwa mara kadhaa kupigana nchini Iraq.  Kyle ambaye aliuawa mwaka 2013 alikuwa mwanachama wa Jeshi la Majini la Marekani ambaye anashikilia rekodi ya kuua watu 160 kati ya walenga shabaha wa Kimarekani.
               

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE