Katika
siku za hivi karibuni kumeibuka tabia ya baadhi ya watu wachache
wasiofahamika kutunga na kusambaza ujumbe kupitia simu za mikononi na
mitandao mbalimbali ya kijamii wenye lengo la kuwatia hofu wananchi,
jambo ambalo ni kinyume cha sheria. Aidha, watu hao wanaosambaza taarifa
hizo wanajifanya kwamba taarifa hizo zimetoka kwenye taasisi za
kimataifa na taasisi zingine zinazoaminika jambo ambalo siyo kweli.
Jeshi
la Polisi nchini linawataka wote wenye tabia hiyo kuacha mara moja na
badala yake, endapo mtu yeyote anayo taarifa ya uhalifu wa aina yoyote
ama kikundi chochote cha uhalifu atoe taarifa hiyo katika kituo chochote
cha Polisi au kupitia simu za makamanda wa polisi wa mikoa ama vyombo
vingine vya ulinzi na usalama ili taarifa hizo ziweze kufanyiwa kazi
haraka.
Aidha,
Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa taarifa zote zinazopokelewa
ili kuhakikisha kwamba usalama wa raia na mali zao unaendelea
kuimarika. Hata hivyo, Jeshi la Polisi halitasita kumchukulia hatua mtu
yeyote atakayebainika kusambaza ujumbe wenye mlengo wa upotoshaji,
uchochezi ama kuwatia hofu wananchi.
Imetolewa na:-
Advera Bulimba -SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment