Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) nchini, Ernest Mangu na viongozi wa dini ya Kiislamu nchini,
wameungana kwa pamoja na kukemea vitendo vya uhalifu.
Viongozi hao wamezitaka familia kutoa malezi bora kwa watoto wao ili
kuondokana na wimbi la watu wanaojiingiza katika vitendo hivyo. Mkuu wa
Jeshi la Polisi Inspekta Jenerali Mangu amesema viongozi wa dini wana
dhamana kubwa katika kuhakikisha vitendo vya uhalifu vinadhibitiwa
nchini kwa kuwaelimisha waumini wao na jamii kwa ujumla juu ya madhara
ya uhalifu.
Mwakilishi wa Mufti Mkuu wa Tanzania
katika kikao hicho ambaye ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Ulamaa katika
Baraza Kuu la Waislamu Nchini (BAKWATA), Sheikh Abubakar Zuberi alisema
kuna haja ya kuziba nyufa za uvunjifu wa amani, ambazo zimeanza
kujitokeza nchini.
Naye Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanazuoni
wa Kiislamu, Sheikh Khamis Mataka alisema uhalifu unaweza kujitokeza
sehemu yoyote na hata ndani ya msikiti, hivyo ni jukumu la viongozi wa
misikiti kuwafichua wahalifu walio ndani ya misikiti.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment