May 21, 2015

Rais Jacob Zuma awaomba radhi raia wa Msumbiji
Hatimaye Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amewaomba radhi raia wa Msumbiji. Rais Zuma amechukua hatua hiyo kufuatia kuuliwa raia kadhaa wa Msumbiji, katika vurugu zilizoambatana na mashambulizi dhidi ya raia wa kigeni nchini humo na kuongeza kuwa, kitendo hicho ni cha kusikitisha mno. Rais Zuma amesema kama ninavyonukuu: "Raia wa Msumbiji ni ndugu zetu na wananchi wa nchi mbili ni watu wa familia moja." Mwisho wa kunukuu. Aidha rais huyo wa Afrika Kusini ameahidi kutojikariri tena mashambulizi dhidi ya wahajiri wa kigeni nchini mwake huku akiahidi pia kuwachukulia hatua kali wahusika wa vitendo hivyo. Itakumbukwa kuwa mnamo tarehe 21 April mwaka huu, Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji aliitaka serikali ya Pretoria kuhitimisha mashambulizi dhidi ya raia wa kigeni nchini humo. Inaelezwa kuwa, raia kadhaa wa Msumbiji walipoteza maisha katika vurugu hizo huku wengine wakipoteza vitu vyao vya thamani. Katika hujuma hizo, makumi ya raia wa kigeni kutoka mataifa mbalimbali hususan ya Afrika waliuawa na raia wa Afrika Kusini waliokuwa na hasira kali wakiwatuhumu wageni hao kuwa chanzo cha wao kukosa ajira.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE