May 08, 2015

 
Ripoti kutoka Nigeria zinasema kuwa wanafunzi watatu wa chuo kimoja cha mafunzo ya biashara, wameuwawa na wapiganaji wa Boko Haram, pale chuo chao kilipovamiwa kazkazini mashariki mwa Nchi hiyo.
Wengine kadhaa walipata majeraha mabaya ya risasi, pale watu wanaoaminika kuwa wa kundi la wanamgambo wa Boko Haram, walipovamia chuo chao na kuanza kumina risasi kiholela.
Mmoja wa washambuliaji alifariki alipojilipua nje ya lango la chuo hicho, nje kidogo ya mji wa Potiskum katika jimbo la Yobe.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE