June 10, 2015

Abou Diaby amewahi kucheza mechi 124 katika miaka tisa aliokuwepo Arsenal 
Mabingwa wa Kombe la FA mara mbili mfululizo Arsenal wamemtema kiungo wao Abou Diaby.
Mchezaji huyo mwenye kipaji, 29, alikuwa akifananishwa na gwiji wa Arsenal Patrick Viera na kocha Arsene Wenger, lakini amekuwa akisumbuliwa na majeruhi.
Diaby amecheza mechi 124 kwa kipindi cha miaka tisa kwenye klabu hiyo na kumuona akisumbuliwa na majeruhi 40.
Kuondoka kwa kiungo huyo kumethibitishwa na maafisa wa Ligi Kuu, na anaungana mshambuliaji wa Japan Ryo Miyaichi, 22, kuondoka Emirates.

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE