June 26, 2015


Uchaguzi Mkuu Tanzania 2015 hauko mbali sana, wasanii wameona huu mwaka haupiti hivihivi… kila mmoja anatangazia nia ya kugombea kwa time yake, Timu ya Leo Tena @CloudsFM walikuwa na staa wa Bongo Movie, Steve Nyerere.. kama umewasikia mastaa wanaoutaka Ubunge safari hii basi liongezee na jina la Steve kwenye hiyo list mtu wangu !!
 
Hekaheka ikaendelea na Steve na mipango yake ya Ubunge wa Kinondoni… Steve Nyerere amesema mpango wake ni huo wa Ubunge wa Kinondoni kupitia CCM.
Steve Nyerere amesema akipita kwenye nafasi hiyo atafanya vitu ambayo watu wengi wanavihitaji, pia yuko tayari kuwataja wala rushwa… kingine anachojipanga nacho ni kushirikiana na viongozi wenzake bila kujali itikadi ya vyama katika kuhakikisha kwamba story za Kinondoni na mafuriko zifike mwisho.
Msikilize Steve hapa alivyojiachia kwenye Hekaheka ya leo…

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE