Vee Money amesema imekuwa heshima kubwa kwake kufuatwa na timu ya jarida hilo ili kumweka kwenye miongoni mwa kurasa za jarida la Essence ambalo lina umaarufu mkubwa nchini Marekani.
“Kwa kuboresha jarida hilo, kila baada ya miaka kadhaa wanafanya global issue na hii ni mara ya kwanza wamerudi Afrika tangia mwaka 1978 na wamechagua kuja Tanzania hivyo ni fursa nzuri. Kwakuwa walifanya utafiti wao, wametafuta watu ambao watakuwa bora kuweka kwenye jarida hilo la global issue,” Vanessa ameiambia Clouds FM.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Essence walidai kuwa wamefurahishwa na kazi za Vanessa Mdee na kuusifia wimbo wake mpya ‘Nobody But Me.’
0 MAONI YAKO:
Post a Comment