July 06, 2015


jerry
Diwani wa kata ya Gongo la Mboto,Jerry Slaa ameainisha mafanikio aliyotekeleza katika kipindi cha miaka mitano tangu achaguliwe kuwa Diwani na Meya wa Manispaa ya Ilala ambapo pia alitimiza ahadi mbalimbali alizokuwa ametoa kwa wakazi wa kata za manispaa ya Ilala.
Slaa alivipatia msaada wa fedha vikundi vya VICOBA alivyokuwa ameviahidi kuvisaidia, jeenereta za kutoa nishati za kuendeshea miradi kwa vikundi kwenye maeneo yasio na umeme, vifaa vya michezo kwa vijana na hati za uthibitisho wa ujenzi wa barabara  zitakazojengwa kwa madiwani wa kata za jimbo la Ukonga.
Slaa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi alitangaza mafanikio hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Shule ya Msingi ya Kitunda iliyopo jimbo la Ukonga  jana ambapo pia alitangaza nia ya kugombea Ubunge wa jimbo la Ukonga kupitia Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
JERRY1
Baadhi ya mafanikio aliyofanikisha katika kipindi cha uongozi wake aliyabainisha kuwa ni katika sekta ya elimu- ambapo mazingira katika shule mbalimbali yameboreshwa, afya-ambapo vituo  vipya vimejengwa na vingine kupatiwa vifaa na dawa,miradi ya maji  na ujezi wa barabara kwenye kata  ya Gongo la Mboto na kata zote za Manispaa ya Ilala.
“Kutokana na mafanikio yaliyopatikana nawaomba wananchi wa jimbo la Ukonga mniunge mkono kwa kinichagua niwe Mbunge wenu katika uchaguzi mkuu ujao ili nizidi kuwatumikia na kushirikiana nanyi kuleta maendeleo katika jimbo hili la Ukonga ambalo bado linakabiliwa na changamoto mbalimbali za maendeleo ”Alisema.
JERRY2
Alisema  wakazi za jimbo la Ukonga  wanahitaji  Mbunge ambaye atakuwa bega kwa bega na wananchi katika harakati za kuwaletea maendeleo wananchi. “Bado tunahitaji kuboresha zaidi huduma za kijamii  kama vile shule, hospitali, maji safi,kubuni miradi ya maendeleo ya akina mama na vijana kwa kuwa naelewa  matatizo ya jimbo hili na baadhi yake nilishaanza kuyavalia njuga nikiwa diwani, mkinichagua kuwa mbunge wenu nitaendeleza safari ya kuleta maendeleo.”


Mkutano huo wa Meya, Jerry Slaa ulihudhuriwa na mamia ya wakazi wengi wa jimbo la Ukonga ambao wengi wao walipokea tamko hilo la kutangaza nia kwa furaha na baadhi ya waliohojiwa walisema kuwa kiongozi huyo anaelewa matatizo ya wananchi wa Ukonga na ni mtu wa watu ambaye amekuwa akitekeleza majukumu yake ya kazi kwa kujali watu wa aina zote.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE