July 16, 2015


Jana akiwa nyumbani kwake Mwanasiasa Mgongwe nchini na Muasisi wa Chama cha Mapinduzi – CCM, Mzee Kingunge Ngombari Mwiru aliongea na waandishi wa habari na kutoa maoni yake juu ya mchakato mzima wa chama chake cha Mapinduzi kilivyompitisha mgombea wao atakayewakilisha chama nafasi ya Urais hapo oktoba 25, ambaye ni Dk. John Pombe Magufuli.
Mzee Kingunge alisema wazi kwamba akuridhishwa na mchakato mzima ulivyokwenda na kulaumu kamati nzima iliyofanya maamuzi hayo.
“Kamati ya Maadili huko nyuma ilikuwa ni chombo cha kuandaa taarifa ili kuisadia Kamati Kuu katok kuwajadili wagombea, lakini safari hii kamati imefanya kazi isiyowahusu kikatiba – kukata majina ya wagombe”, alisema Mzee Kingunge.
Mzee huyo alisema kwamba Kamati ya maadili ya CCM yenyewe imekosa maadili ya kuheshimu katiba na taratibu za chama na wala haikuwa na madaraka ya kupeleka majina 5 kwenye kamati kuu, ambayo ilipaswa kuhoji wagombea wote 38.
Pia Mzee, Kingunge alionyesha wazi chaguo lake kuwa ni Mh. Edward Lowassa kwani tangu mwanzo alionyesha kupendwa na watu.
Lakini licha ya Lawama zote hizo Mzee Kingunge alisema ataendelea kuwa mwanachama muadilifu ndani ya chama hicho.

Related Posts:

  • Magufuli ampa kazi Kikwete Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (Chancellor of the Univ… Read More
  • Tumekuwekea hapa magazeti ya leo Ijumaa January 22, 2016 Leo Ijumaa January 22, 2016 tunakuletea habari katika magazeti yetu kama yalivyo tufikia. Share na mwenzio … Read More
  • Watu 20 wauawa hotelini              Magari yaliyokuwa yameegeshwa nje ya hoteli hizo yaliharibiwa vibaya Waziri wa usalama wa ndani nchini Somalia amesema watu 20 walifariki baada y… Read More
  • Anti Sadaka awafunda wanawake           Mwanasaikolojia Anti Sadaka akitoa Mada kwenye Mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa Mkoa wa Mwanza yanayoendesha na  Taasisi ya Manjano foundation yanaoen… Read More
  • Uchaguzi Zanzibar,i ZEC wataja Tarehe Tume ya Uchaguzi ya zanzibar ZEC imetangaza tarehe rasmi ya kurudiwa kwa uchaguzi  mkuu visiwani humo kuwa ni  2o March 2016 Taarifa hiyo imetolewa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar imeb… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE