Watu wanne wamefariki dunia na 21 kujeruhiwa baada ya basi aina ya Isuzu
kugonga treni ya abiria iendayo bara katika kilomita 276/0 kati ya
Stesheni za Kimamba na Kilosa mkoani Morogoro saa 11:25 asubuhi leo
Julai 01, 2015. Wahanga walipakiwa katika treni hiyo na kukimbizwa
katika Hospitali ya Wilaya ya Kilosa.
Basi lilohusika ni lenye namba za
usajili T837CTM Isuzu Coaster linalomilikiwa na Feisal A. Khuwel wa
Kilosa.Taarifa kutoka eneo la tukio limefafanua kuwa waliofariki ni
wanaume wawili, mwanamke mmoja na mtoto wa miaka minne. Katika majeruhi
21 wako wanaume 14 na Wanawake 7 ambao wanaendelea na matibabu katika
Hospitali ya Wilaya ya Kilosa! Treni ya abiria imeondoka katika Stesheni
ya Kilosa saa 3 asubuhi kuendelea na safari yake kwenda Bara. Uongozi
wa TRL unawapa pole Ndugu wa Marehemu kwa msiba mkubwa uliowakuta bila
ya kutarajiwa na pia inawaombea Marehemu kwa Mola awape mapumziko ya
Amani peponi Amina! Hali kadhalika inawaombea majeruhi wapate afueni ya
haraka ili warejea katika shughuli zao za kawaida kwa familia zao na
Taifa letu.
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Elias Mshana Dar es Salaam! Julai 01, 2015
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Elias Mshana Dar es Salaam! Julai 01, 2015
0 MAONI YAKO:
Post a Comment