Timu Manchester United imeshinda mchezo wa duru ya kwanza wa kufuzu kucheza michuano ya Champions League kwa magoli 3 - 1 dhidi ya Club Bruges hapo jana uwanjani Old Trafford.
Michael Carrick alijifunga dakika ya 8 tu ya mchezo huo na kuwapa uongozi wageni hao wa Ubelgiji.
Alikuwa Mchezaji mpya wa United, Memphis Depay aliyesawazisha goli hilo dakika ya 13 ya kipindi cha kwanza.
Mdachi huyo aliyekabidhiwa jezi namba saba ya Old Trafford alirudi tena dakika ya 43 na kufunga goli la pili na kuwafunga mdomo mashabiki wa Bruges waliosafiri kutoka Ubelgiji kuishuhudia timu yao.
Akitokea benchi, Marouane Fellaini akafunga kwa kichwa goli la tatu dakika ya 90 ya mchezo huo na kufanya ubao usomeke 3 - 1.
Bruges walimaliza pungufu usiku wa jana wakiwa wachezaji 10, baada ya mchezaji wake Brandon Mechele kuonyeshwa kadi ya pili ya manjano.
Matokeo mengine ya mechi za jana ni BATE (Blr)ilishinda goli 1 - 0 dhidi ya Partizan (Srb), huku Lazio (Ita) ikipata matokeo 1 - 0 mbele ya Bayer Leverkusen (Ger), ambapo pia timu ya Sporting (Por) ikashinda magoli 2 - 1 dhidi ya CSKA Moscow (Rus) na FC Astana (Kaz) ikashinda ushindi wa goli 1 - 0 ikiifunga APOEL (Cyp)
0 MAONI YAKO:
Post a Comment