August 02, 2015


 MGOMBEA wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia chama cha UPDP, Fahmi Dovutwa, (kulia), akipokea mkoba wenye fomu za uteuzi wa kuwania kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2015, za Tume hya Taifa ya Uchaguzi, (NEC), kutoka kwa afisa mwandamizi wa tume hiyo, makao makuu ya NEC, jijini Dar es Salaam jana asubuh Agosti 1, 2015. Dovutwa amekuwa mgombea wa kwanza kuchukua fomu hizo na kazi iliyo mbele yake ni kutafuta wadhamini 200 ambao ni raia wa Tanzania wenye shahada za kujiandikisha kupiga kura kwenye uchaguzi huo. Dovutwa alifuatana na mgombea mwenza wake, Hamad Mohammed UIbrahim na wanachama wachache wa chama hicho

             

 Barua ya kutoka chama cha UPDP inayomtambulisha Dovutwa, (kushoto), kuwa ndiye mgombea wake wa kiti cha Rais zikikaguliwa na afisa mwandamizi wa tume hiyo, William Kitebi.                              

               

 Fahmi Dovutwa, mgombea wa kiti cha Rais kupitia UPDP

               

Mgombea mwenza wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia UPDP, Hamad Mohammed Ibrahim

     

Mgombea kiti cha Urais kupitia TLP, Maxmillian Lyimo, (kulia), akipokea mkoba wenye fomu za uteuzi wa kuwania kiti hicho za Tume ya Taifa ya Uchaguzi 

Mgombea kiti cha urais kupitia TLP, Maxmillian Lyimo, akionyesha mkoba wenye fomu za uteuzi za tume ya taifa ya uchaguzi, NEC, baada ya kukabidhiwa.

              

Maxmillian Lyimo, mgombea kiti cha Rais wan Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia TLP. 
PICHA KWA HISANI YA K-VIS BLOG.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE