
Mwanahamisi Muyinga.

Makada wa Wawili wa Chadema
Mbunge viti maalumu anayemaliza muda wake Chuki Abwao na aliyekuwa mmoja
wa watia nia Jimbo la Kalenga aliyeshindwa kwenye kura za maoni
wameibuka kidedea kwenye kura za maoni kuwania ubunge kupitia chama cha
ACT Wazalendo.
Makada hao waliibuka washindi
kwenye uchaguzi uliofanyika juzi Chuki Abwao akishinda jimbo la Iringa
mjini na Mwanahamisi Jimbo la Kalenga.
Makada hao sasa wanasubiri
vikao vya juu vya chama ili kuidininisha kuwania ubunge na ikiwa vikao
hivyo vitabiri Chuki atapambana na Mbunge wa Iringa Mjini anayemaliza
muda wake Mchungaji Peter Msigwa, Mgombea ubunge kupitia CCM anayesubiri
vikao vya juu vya chama hicho Frederick Mwakalebela na wagombei wa
vyama vingine ikiwa watajitokeza.
Wakati Chuki akitarajia
kupambana na wagombea hao Mwanahamisi anatarajia kupambana na Mbunge wa
sasa anayemaliza muda wake Godfrey Mgimwa ambaye pia ni mshindi wa kura
za maoni na kada mmoja kati ya Lucas Mwenda na Mussa Mdede wote kutoa
Chadema ambao walipata kura 64 kila mmoja.
Katika uchaguzi uliofanyika
kwenye ofisi za ACT Wazalendo Mkoa wa Iringa Chuki aliwashinda
washindani wake Daud Masasi na Dk Ben Kapwani kwa baada ya kupata kura
23 akimuacha Masasi kwa kura mbili baad aya kupata kura 21 huku Dk
Kapwani aliyetangaza kujitoa akipata kura tatu.
Katika uchaguzi uliofanyika
kwenye eneo la Kihodombi kata ya Mlandege Mwanahamisi aliibuka mshindi
kwa akupata kura 10 akifuatiwa na Daniel Mwangili aliyepata kura 7 huku
Edward Mtakimwa na Kiduo Mgunga wakipata kura 3 kila mmoja.

Chuki Abwao.

Hata hivyo matokeo ya Iringa
mjini yalipata ukakasi baada ya mmoja wa wagombea ambaye ni katibu
Mwenezi wa ACT mkoa wa Iringa akigomea kusaini matokea hayo kwa madai
kuwa yaligubikwa na vitendo vya rushwa.
Hata hivyo madai hayo
yalipingwa na Mwenyekiti uchaguzi Mjini Iringa Placid Kamonga aliyesema
uchaguzi huo ulifanyika kwa uwazi na demokrasia ya kweli kwa kuwa kura
zilipigwa na kuhesabiwa kwa uwazi.
Mwenyekiti wa ACT mkoa wa
Iringa Kapwani alisema ni vema Masasi akasaini matokeo na kuendelea na
mchakato wake kupinga matokeo ambao kwa mujibu wa waraka wa chama hicho
mtu anayepinga matokeo atatakiwa kufanya kuwasilisha malalamiko yake
ndani ya siku saba tangu kufanyika kwa uchaguzi.
Kwa upande wake Chuki ambaye
alishinda uchaguzi huo aliwashukuru wapiga kura kwa akumuaamini na
kueleza kuwa atahakikisha anafanya kazi ya kukijenga chama hicho
kichanga kinachoingia katika uchaguzi mkuu kwa mara ya kwanza tangu
kusajiliwa kwake.
Naye Mwanahamsi aliwashukuru
wapigakura kwa kumuamini na kufafanua kuwa atahakiksha anatumia taalamu
yake ya kilimo kuinua maisha ya wakazi wa Kalenga.
Katibu wa chama hicho Mkoa wa
Iringa Aram Mbilinyi aliwataka makada wote wa ACT Wazalendo kuungana
pamoja kushirikiana na aliyeshinda ili kutafuta ushindi kwenye uchaguzi
kwa kuwa ushindi wa matokeo yaliyotokana na kura za maoni na y a watu
wote.
“Hapa hakuna mshindi sisi sote
tumeshinda wito wangu kwenu tuungane pamoja kuhakikisha tunawaunga mkono
hawa mama zetu katika kipindi chote cha kampeni tukiwa na imani kuwa
wakishinda wao tumeshinda sote”alisema Mbilinyi.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment