August 29, 2015

Wasichana wapatao 38 wamekufa katika ajali ya gari nchini Swaziland wakati walipokuwa wakisafiri kwenda kwenye sheria ya kitamaduni.

Shirika la kutetea haki za binadamu nchini Swaziland, Solidarity Network limesema wasichana hao waliokufa walikuwa wamejeruhiwa vibaya wakati gari lao lilipogongana na gari jingine siku ya Ijumaa.

Walikuwa njia kwenda katika jumba la mfalme wa nchi hiyo katika ngoma maarufu ya kitamaduni.

Kila mwaka kiasi cha wasichana wapatao elfu arobani hushiriki kwenye sherehe hizo za kitamaduni za siku nane.
Hupita mbele ya mfalme wakiwa nusu uchi. Mashirika ya kutetea haki za binadamu wamekuwa wakipinga sherehe hizo kwa kusema zimepitwa na wakati na ni za king'ono.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE