Mwigizaji maarufu, Kingwendu amenusurika kifo baada ya ajali mbaya ya gari iliyotokea leo Wilayani Kisarawe.
Kingwendu amekumbana na ajali hiyo akiwa katika kampeni zake za kuwania ubunge katika Jimbo la Kisarawe.
Mwigizaji huyo anawania nafasi hiyo kupitia Chama cha Wananchi (CUF) na kampeni zake zimekuwa zikipamba moto.
Msemaji wa Kingwendu, Msanii mwingine, King Sapeto amesema aliyeumia ni mtu mmoja tu aliyeumia anajulikana kwa jina la Big.
“Big ndiye pekee aliyepata majeraha,” alisema King Sapeto bila ya kutoa maelezo zaidi.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment