September 05, 2015

Ustadh Jafari Atiki, kutoka katika taasisi ya Darul Hadith Islamic
Viongozi wa dini mkoani Mtwara wamewataka waandishi wa habari kutimiza wajibu wao kwa kuielisha jamii namna ya kuishi na kutenda haki ili kudhibiti vitendo vya kifisadi vinavyofanywa na baadhi ya watu.
 Akizungumza jana , Mchungaji Zakaria Lyakungi, kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania, jimbo la Pwani, amesema ni wajibu wa waandishi kuikemea jamii bila woga iwapo kutakuwa na vitendo viovu.
Kwa upande wake, Ustadh Jafari Atiki, kutoka katika taasisi ya Darul Hadith Islamic, amesema waandishi wa habari ni kama viongozi wa dini kwa namna wanavyoaminiwa na jamii, hivyo hawatakiwi kuegemea upande wowote katika ufanyaji wa kazi zao.
Naye, makamu mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mtwara (MTPC), Jimmy Mahundi, amewasisitiza waandishi kujihepusha kuwa chanzo cha matatizo na baadala yake kuwa msaada kwa jamii inayokumbwa na matatizo na kuhitaji msaada wao.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE