October 09, 2015

Mgombea urais kupitia chama cha TLP Macmillan Lyimo amesema anaunga mkono kauli ya mwenyekiti wake wa chama Mh. Augustine Mrema ya ‘kumpigia debe’ mgombea wa chama cha mapinduzi CCM, Dk John Magufuli, kwa madai kuwa hayo ni maamuzi yake binafsi.

Akizungumza na East Africa Radio mchana  huu, Lyimo amesema kuwa kauli hiyo haijatolewa na mkutano wowote wa chama, bali ni maoni binafsi kwa kuwa mwaka huu watanzania wanachagua mtu na siyo chama na kwamba jambo alilofanya Mrema si jipya wa la ajabu.

“Hili jambo siyo la ajabu, hata Marekani, Colin Powell alitangaza kumuunga mkono Obama licha ya kuwa chama tofauti, Mrema amesema hivyo kwa kuwa anajua looser siyo yeye, tumesimamisha wagombea ubunge nchi nzima, na yeye ni mmoja wapo, kwahiyo hilo halinipi shida” Amesema Macmillan Lyimo

Kuhusu mahusiano kati yake na mwenyekiti huyo, Lyimo amesema kuwa mahusiano ndani ya chama hicho ni mazuri na hakuna ugomvi wowote.

“Tunaendelea kushirikiana kama kawaida, na hata kampeni zangu nilianzia kwake na nitafungia jimboni kwake” kauli ya Lyimo
Kuhusu nafasi yake ya ushindi, Lyimo amesisitiza kuwa yeye ndiye atakayeshinda urais mwaka huu, na kamwe Rais hatoki CCM


“Magufuli hawezi kushinda, nafasi kubwa ya ushindi ninayo mimi, hata Magufuli anajua kuwa mimi napinga huo mwenge kwenye picha yake, hiyo ni ishara ya uchawi, na uchawi wake utashindwa mwaka huu”.Amesema mgombea huyo.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE