October 04, 2015

Gari alimopata ajali Mch mtikira 

Mwenyekiti wa chama cha siasa (Democratic Party - DP) nchini Tanzania, Mchungaji Christopher Mtikila amefariki dunia alfajiri ya leo katika ajali ya gari iliyotokea kwenye kijiji cha Msolwa, Chalinze mkoani Pwani, alipokuwa safarini akitokea kwake mkoani Njombe.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Jafar Ibrahim amethibitisha hilo na kusema watu wengine watatu waliokuwa katika gari hilo wamekimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE