November 24, 2015


BEN 1
.Wanamuziki Ben Paul na Fid Q wanaoshiriki kwenye  onyesho la Coke Studio wakiwa katika picha ya pamoja na washabiki wao wakati wa uzinduzi wa onyesho hili jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
BEN 2
Sehemu ya wafanyakazi wa kiwanda cha Coca Cola Kwanza wakifuatilia onyesho la Coke Studio.
BEN 3
Msimu wa Coke Studio umewahusisha pia wanafunzi mashuleni kuonyesha vipaji vyao kama anavyoonekana mwanafunzi akionyesha kipaji cha kucheza katika moja ya tamasha la Coke Studio lililofanyika mjini Mwanza hivi karibuni.
Mwanamuziki nguli wa Bongo Fleva nchini Ben Paul amesema kuwa ushiriki wake katika onyesho la Coke Studio ni moja ya mafanikio katika safari yake ya muziki.
Katika mahojiano aliyoyafanya wiki hii kuhusiana na ushiriki wake katika onyesho hili maarufu linaloendeshwa na kampuni ya Coca-Cola na kushirikisha kolabo za wanamuziki mbalimbali wa Tanzania na nje ya nchi alisema anajivunia ushiriki wake katika onyesho hili na ameweza kujifunza mengi kuhusiana na fani ya muziki.
“Japo hapo awali nimewahi kushinda tuzo mbalimbali za muziki lakini ushiriki wangu katika onyesho hili  kubwa la kimataifa ni moja ya mafanikio yangu makubwa katika safari yangu ya muziki.
Alisema anajisikia fahari  kufanya kolabo kwa kushirikiana na mwanamuziki Wangechi kutoka nchini Kenya katika msimu huu wa Coke Studio ambapo kwa hapa nchini onyesho hilo linarushwa kila siku ya Jumamosi saa kumi na mbili jioni kupitia luninga ya Clouds.
Ben Paul alisema onyesho la Coke Studio linahamasisha vijana kujiamini na kuonyesha vipaji vyao na aliwataka vijana wenzake kujiamini na kutokata tamaa iwapo wanataka kutimiza ndoto zao na kufanikiwa katika maisha.
Alisema katika safari yake ya muziki amekutana na changamoto nyingi mojawapo ikiwa ni kunyimwa nafasi ya kurekodi nyimbo zake na waandaaji mbalimbali wakiamini kuwa hakuwa na uwezo wa kuimba lakini licha ya kufanyiwa hivyo aliendelea kupambana mpaka kufanikiwa kufika alipo sasa.
“Ninachotaka kuwaambia ni kwamba, mfano, kwa wale wenye vipaji vya kuimba, kitu kikubwa unachotakiwa kufanya ni kuwa na nyimbo nyingi ambazo, hata ukirekodi moja isipofanya vizuri, unatoa nyingine ili kuhakikisha unaendelea kusikika masikioni kwa watu”, alisema
Aliwaasa vijana wa jinsia zote  kujiamini na kuondokana na dhana kwamba jinsia fulani ndio wanaweza  kufanya kitu fulani na kusisitiza kuwa kila mtu ana kipaji na anaweza kufanya mambo makubwa.
Alimalizia kwa kuwapongeza wanamuziki wenzake kutoka Tanzania ambao wako nao katika msimu huu wa tatu wa Coke Studio mwaka huu. Wanamuziki hao ni Fid Q ambaye amefanya kolabo (mash-up) na Maurice Kirya na Vanessa Mdee ambaye amefanya kolabo (mash-up) na mwanamuziki 2face kutoka Nigeria na Ali Kiba ambaye amefanya Kolabo  na mwanamuziki Victoria Kimani.
Lengo kuu la Coke Studio Afrika ni kuwakutanisha kwa pamoja wasanii wenye mbalimbali wa Afrika na kuimba nyimbo ambazo zina vionjo tofauti hivyo kuongeza msisimuko. Lakini vilevile kutoa fursa kwa wasanii wachanga  kushirikiana na wasanii wakubwa ili kuwapa changamoto ya kuongeza ujuzi katika kazi zao na kuzidi kukuza vipaji vyao
Onyesho la Coke Studio linarushwa kila siku ya Jumamosi saa kumi na mbili jioni kupitia luninga ya Clouds. Pia unaweza kusikiliza kipindi cha Coke Studio kwenye Clouds FM kila Jumamosi saa nne asubuhi.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE