December 02, 2015

waziri
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambaye anamaliza muda wake, Bw. Juma-Alfani Mpango.
Akizungumza na balozi Mpango leo ofisini kwake, Magogoni jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu amemshukuru balozi huyo kwa pongezi zake na kumuomba aendelee kuwa balozi mzuri wa kuitangaza Tanzania hata baada ya kurejea nyumbani na kutumia fursa hiyo kuwaombea heri wananchi wa DRC pamoja na Rais Joseph Kabila katika maandalizi ya uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanyika nchini humo mwakani.
Kwa upande wake, Balozi Mpango ambaye alisema amekaa hapa nchini kwa miaka 12, alimweleza Waziri Mkuu kwamba amejifunza mengi kutoka kwa viongozi wa Tanzania , kubwa likiwa ni uchapakazi na unyenyekevu.
Balozi Mpango ameomba mahusiano ya nchi hizi mbili yaendelezwe, kwani DRC imekuwa ikinufaika na matumizi ya bandari ya Dar es Salaam katika kusafirishia bidhaa zake kwenda nchi za nje

Chanzo: Channel Ten

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE