January 10, 2016

Zaidi ya wachungaji hamsini wa kanisa la Anglikana Tanzania dayosisi ya Victoria Nyanza (DVN) wametangaza kumfukuza kazi ya uaskofu, askofu Bonifasi Kwangu wa dayosisi hiyo kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na ubadhirifu wa fedha pamoja na mali za kanisa hilo.

Tamko hilo la wachungaji 53 wa dayosisi hiyo limesomwa mbele ya waumini wa kanisa kuu la mtakatifu Nicholas wakati wa ibada ya jumapili na mchungaji Andrew Kashilimu, ambaye pia ni mwenyekiti wa nyumba ya wahudumu.

 

Kufukuzwa kazi ya uaskofu kwa askofu Bonifasi Kwangu aliyehudumu katika dayosisi hiyo ya Victoria Nyanza (DVN) kwa miaka minane, kuanzia mwaka 2008 hadi kufikia leo, kunafanya jumla ya maaskofu waliowahi kufukuzwa na kanisa hilo kufikia wawili, akiwemo mtangulizi wake marehemu John Changaye ambaye alifukuzwa uaskofu mwaka 2007 kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha na mali za kanisa hilo.

 

Askofu Bonifasi Kwangu amevuliwa wadhifa huo akiwa nchini Marekani ambako amekaa kwa zaidi ya mwezi mmoja.

 

Kanisa la Anglikana Tanzania dayosisi ya Victoria Nyanza (DVN) lina jumla ya wachungaji sitini na zaidi ya waumini laki sita katika makanisa yake.

Related Posts:

  • Butiku "wazanzibar msikubali kurudia uchaguzi" Taasisi ya mwalimu Nyerere imeitaka tume ya uchaguzi ya Zanzibar ZEC kufanya kazi kwa kuzingatia katiba ya nchi na sheria na sio kutanguliza mbele maslahi binafsi ya kisiasa hatua ambayo inaweza kusababisha machafuko na umwa… Read More
  • Wasanii Bungeni watimize waliyoahidi - Stereo  Msanii Stereo amewataka wasanii waliofanikiwa kuchaguliwa kuingia Bungeni, wakatimize wajibu wao kwa kuyatekeleza yale waliyoyaahidi kipindi cha kampeni, na si kuyapuuzia baada ya ushindi. Stereo ameyasema … Read More
  • Alichokiongea DR. Magufuli baada ya kushinda nafasi ya UraiS Baada ya Rais mteule wa Tanzania, Dr. John Magufuli na Makamu wake Mama Samia Suluhu Hassan kukabidhiwa cheti na Tume ya Uchaguzi NEC, safari ilianza toka Ukumbi wa Diamond Jubilee Upanga mpaka Ofisi za CCM mta… Read More
  • Obama aing'oa Burundi Mshirikishe mwenzako Image copyrightAFPImage captionMarekani imeiondoa Burundi kutoka kwenye mikataba yake ya kibiashara AGOA iliyowezesha mataifa ya Afrika kuingiza bidhaa zao katika soko la Marekani bila kulipa kodi. Mare… Read More
  • Maafisa wa kituo cha kukusanya taarifa cha TACCEO wakamatwa Wakili Imelda – Lulu Urio Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC. Chanzo:MOE BLOG Mtandao wa Asasi za Kiraia za Kuangalia chaguzi nchini jana ulipata pigo katika mwendelezo wake wa kukusanya taarifa juu ya mchakato wa… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE