January 18, 2016

Bei ya sasa ta mafuta ndiyo ya chini zaidi tangu mwaka 2003

Bei ya mafuta imeshuka hadi chini ya dola 28 kwa pipa licha ya kuwepo hofu kuwa kuondolewa kwa vikwazo vya Iran kutashusha bei zaidi kutokana na tatizo la uzalishaji mkubwa.

Bei za mafuta yasiyosafishwa katika soko la kimataifa zilishuka chini ya dola 27.67 kwa pipa ambayo ni bei ya chini zaidi tangu mwaka 2003 kabla ya bei tena kupanda kidogo na kuuzwa kwa dola 29,25 kwa pipa.

Bei ya mafuta yasiyosafishwa nchini Marekani ilishuka chini ya dola 29 kwa pipa hadi dola 28.86.

Kuanza kuuzwa kwa mafuta ya Iran kutachangia bei kushuka zaidi

Kuondolewa kwa vikwazo vya Iran ina maana kuwa mapipa nusu milioni zaidi yatazalishwa kwa siku kulingana na wadadisi.

Uamuzi wa kuiondolea Iran vikwazo uliafikiwa siku ya Jumapili baada ya shirika la kimataifa la kudhibiti nishati ya nuklia IAEA kusema kuwa Iran imetekeleza makubaliano yanayozuia isiunde zana za nuklia.

Iran inachukua nafasi ya nne kati ya nchi zenye hifadhi kubwa zaidi ya mafuta duniani.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE