January 20, 2016

Msanii Joh Makini kutoka kundi la Weusi amesema anategemea kuja na video mbili za nyimbo zake za zamani, Kilimanjaro aliyomshirikisha Lady Jaydee na Nikumbatie aliyomshirikisha Fundi Samwel kwa kuwa anaamini nyimbo hizo zinaweza kufanya vizuri zaidi kimataifa.

Rapa huyo aliyeachia wimbo wa Don’t Bother miezi kadhaa iliyopita, amesema hayo kwenye kipindi cha Siz Kitaa cha Clouds Tv kuwa ana imani kuwa kazi hizo zinaweza kwenda mbali zaidi.

“Sina kitu ambacho nimekosa katika video zilizopita labda quality ambazo zinapatikana sasa hivi kama ningezipata wakati ule video zingeenda mbali zaidi”, alisema Joh.

“Sina mpango wa kurudia video ya wimbo wowote lakini nina mpango wa kufanya video za nyimbo zangu ambazo hazikupata video, Nikumbatie na Kilimanjaro, ni ngoma ambazo zilistahili kupata video kwasababu ni nyimbo ambazo naona zikipata video zitaenda mbali zaidi. Pia standard ya video zangu nataka iwe inaenda mbele, kwahiyo watu wategemee kazi nzuri"

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE