Drogba alijiunga na meneja mpya wa Chelsea Guus Hiddink kutazama mechi Stamford Bridge mwezi Desemba
Klabu ya Montreal Impact imesema nyota wa zamani wa Chelsea Didier Drogba atasalia katika klabu hiyo, na kusitisha uvumi kwamba huenda akarejea Stamford Bridge.
Montreal wamesema Drogba ataungana na wachezaji wenzake kwa mazoezi ya kabla ya kuanza kwa msimu.
Muda mfupi baadaye, mchezaji huyo wa miaka 37 aliandika kwenye Twitter: “Niko safarini kwenda Qatar kujiandaa kwa mwanzo wa msimu.”
Drogba alifanya mazungumzo na Chelsea mwezi Desemba kukiwa na uvumi kwamba huenda atarejea Chelsea kufanya kazi pamoja na wakufunzi.
Wakati huo, Montreal, wanaocheza Ligi Kuu ya Marekani na Canada (MLS) ilikiri kwamba Drogba alikuwa ameelezea nia ya kutaka kuisaidia Chelsea na kwamba hali ilikuwa haimo mikononi mwao tena.
Image copyrightBBC World Service
Lakini Drogba alipuuzilia mbali habari kwamba alitaka kuwa mkufunzi na kuandika kwenye Twitter: “Bado sijatangaza kwamba nastaafu.”
Sasa inaonekana kana kwamba huenda Drogba akatumikia mkataba wake Montreal ambao unamalizika mwisho wa mwaka huu.
Msimu uliopita, Drogba ndiye aliyekuwa mfungaji mabao bora wa Montreal, akiwafungia mabao 11.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment