January 22, 2016

 

Mchambuzi wa masuala ya kisiasa na mwanasheria kutoka Chama cha Wananchi (CUF) Julius Mtatiro amesema Bunge limemwangusha Rais Magufuli kwa kuchagua kamati dhaifu katika kamati zilizotangazwa hivi karibuni.
Akielezea masikitiko yake katika kipindi cha Hot Mix cha EATV Mtatiro amesema kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) imewekwa wabunge wageni kutoka upinzani na kamati hiyo inatakiwa kuongozwa na mbunge kutoka upinzani hivyo lengo la kuisimamia serikali halijapewa kipaumbele.
''Rais Magufuli alipolihutubia bunge aliomba kupewa ushirikiano wa hali ya juu kuchagua wabunge wapya wa kusimamia hesabu za serikali ni kuwapa wabunge hao mzigo mzito, kamati hii ilikuwa ikiongozwa na Zitto na serikali iliona uwezo wake ndiyo maana wametafuta watu ambao hawana uzoefu jambo ambalo sii zuri'' Amesisitiza Mtatiro.
Mtatiro ameongeza kuwa ''Spika Ndugai hakuhitaji elimu ya chuo kikuu katika kufanya uteuzi wa kamati hizi na sidhani kama kuchagua kamati dhaifu kama hizi kunamaanisha dhana ya Rais Magufuli ya hapa kazi tuu''.
Kuhusu Tume ya uchaguzi Zanzibar kutangaza tarehe ya uchaguzi Mtatiro amesema kilichofanyika Zanzibar ni makusudi matupu na kama CUF haitashiriki katika uchaguzi huo ni wazi kuwa kutakuwa na sintofahamu kisiwani humo.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE