January 17, 2016

        jada pinket

Je,Jada Pinket mkewe nyota wa filamu Will Smith hatashiriki katika tuzo za Oscar?

Nyota huyo aliandika katika mtandao wake wa Tweeter siku ya jumamosi akionyesha kukasirishwa na ukosefu wa watu wa rangi tofauti miongoni mwa wale walioteuliwa kuwania tuzo za Oscar.

Ujumbe wa Jada pinket

Katika msururu wa ujumbe huo katika mtandao wa Twitter,Jada mwenye umri wa miaka 44 alishangazwa alipogundua kwamba hakuna nyota weusi walioteuliwa katika orodha za juu wakati uteuzi huo ulipofanywa siku ya Alhamisi.

''Katika tuzo za Oscar watu weusi hukaribishwa kutoa tuzo mbali na kuwatumbuiza wageni'',lakini hatutambuliwa kwa usanii wetu ,alisema Jada.

''Je watu weusi wajiondoe katika tuzo hizo kwa jumla'',?Aliongezea.

Will Smith na mkewe Jada Pinket

''Watu wanafaa kutuchukulia vile tutakavyo',kwa heshima kubwa''.

Kwa mwaka wa pili mfululizo,hakuna watu weusi walioorodheshwa katika orodha ya nyota bora au nyota bora mwanamke, ama hata nyota msaidizi.

Tangazo la walioteuliwa lilifuatiwa mara moja na hisia kali katika mitandao ya tweeter ikiwemo matumizi ya #OscarSoWhite

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE