January 18, 2016

Producer maarufu wa Tanzania kwenye muziki wa bongoflevaNahreel ameingia kwenye top stories za leo kwenye Dstv.com baada ya kukataa kumpa beat yake staa mmoja wa hip hop nchini Kenya.

Nahreel ambaye mikono yake ina hits tano kwenye nyimbo 20 za Clouds FM Top 20ameweka wazi kuwa alimkatalia kurekodi baada ya kugundua kwamba jamaa hakuwa na pesa.

 "Jamaa alikuja studio, sitaki kumtaja jina ila aliniambia bwana inabidi tufanye kazi pamoja, tutengeneze wimbo... mi nikakubali na kazi ikaanza ila baada ya kumaliza kusuka kila kitu mwishoni akasema hana pesa ya kulipia beat, nikamkatalia."

 

Nahreel aliongezea, "Alijua sababu yeye analo jina kubwa labda ningempa beat for free ila ukweli ni kwamba sina hiyo, mimi nafanya biashara.... kila msanii unayemsikia juu ya beat ya Nahreel ujue amelipia, akaniambia basi naomba beat niende nayo nitakutumia pesa nikamwambia hapana, sifanyagi hivyo, tafuta pesa njoo lipia nitakutunzia beat yako."

 

Bei moja ya Nahreel inapatikana kuanzia shilingi milioni moja mpaka milioni moja na nusu za Kitanzania na mara nyingi Nahreel anapenda kufanya kila kitu kwenye studio yake, yani hapendi wala hataki kuuza beat peke yake, anapenda asimamie kazi beat yake itendewe haki na msanii hata kama ameiuza.

Source:Dstv.com


0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE