January 17, 2016

 
Manejimenti ya sahara media group ikizungumzia juu ya  taarifa hizo imesema haijapata barua au taarifa rasmi yeyote kutoka mamlaka ya mawasilano Tanzania TCRA  ya kutakiwa kufunga vyombo vyake,

Imesema wameshtushwa na taarifa hiyo ikizingatiwa kwamba wamekuwa wakilipia leseni ada zake na ada za masafa kwa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni miatano hadi kufikia mwezi October 2015.

Wamesema yamekuwapo mawasiliano ya mara kwa mara kati ya TCRA akanda ya Mwanza, makao makuu na sahara media group limited nakukubaliana juu ya utaratibu wa malipo ya ada husika.

lakini menejimenti imeshangazwa na hatua hiyo ya TCRA kutanagaza kuvifungia vituo vyake kupitia kutano wa  vyombo vya habari bila kujali athari zakufungia vyombo vya kitaifa kwa walaji na watoa huduma.

Sahara media group limited imekuwa ikilalamikia utozwaji wa ada kwa dola za kimarekani jambo ambalo limekuwa likipandisha ada hizo kila mara na kufanya ulipwaji wa ada hizo kibajeti kukwama kwama.

Menejimenti pia imelaani kwa taarifa hiyo kutolewa mwishoni wa wiki nakuvipa vituo husika siku mbili tu kukamilisha ulipaji ada wakijua dhahiri jumamosi na jumapili sio siku za kazi.

Menejimenti ya star tv  inawaondoa wasiwasi watazamaji na wasikilizaji wake,  hatua  thabiti zitachukuliwa ili kumaliza tatizo hili kwa sahara media group limited  na TCRA Kwa Kufuata Misingi Ya Sheria, Kanuni Na Maridhiano

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE