January 14, 2016

Rene Angelil alihudumu kama meneja wa Celine Dion hadi 2014

Rene Angelil, mume wa mwanamuziki mashuhuri duniani Celine Dion, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 73, mwanamuziki huyo ametangaza.

Bw Angelil, aliyemuoa Dion mwaka 1994 na wakajaliwa watoto watatu, amekuwa pia akihudumu kama meneja wake.

Alifariki akiwa nyumbani kwao Las Vegas baada ya kuugua saratani.

Dion alichukua likizo kutoka kwenye muziki kwa vipindi viwili ili kumtunza Angelil baada yake kupatikana na saratani ya koo mwaka 2000.

Bw Angelil alizaliwa mjini Montreal mwaka 1942.

Baada ya kuwa meneja wa makundi kadha nchini Canada, aliombwa na wazazi wa Dion awe meneja wake mwanamuziki huyo alipokuwa na umri wa miaka 12 pekee.

Mwaka jana, Dion aliambia gazeti la USA Today kwamba alikuwa akijiandaa kwa kifo cha mumewe.

“Ikifika, itafika tu,” aliambia gazeti hilo Agosti 2015.

“Lakini kibarua change kikubwa kitakuwa kumwambia mume wangu kwamba tuko sawa. Nitawatunza na kuwalea watoto wetu. Utatutazama kutoka ulimwengu mwingine.”

Gazeti la Montreal Gazette linasema Bw Angelil aliweka rehani nyumba yake ili kupata pesa za kufadhili albamu ya kwanza ya mwanamuziki huyo.

Dion amerekodi albamu 25 studioni na ndiye mwanamuziki wa tano kwa kulipwa pesa nyingi zaidi, utajiri wake ukikadiriwa kuwa $630m (£437m).

Mwaka 1999, wimbo wake My Heart Will Go On, uliotumiwa katika filamu ya Titanic, ulishinda tuzo mbili za Grammy.

Amekuwa akitumbuiza mara kwa mara katika ukumbi wa The Colosseum, Caesars Palace mjini Las Vegas tangu 2003.

Alianza tena kutumbuiza mashabiki wake mwaka jana baada ya kupumzika mwaka mmoja kumtunza Bw Angelil, ambaye aliacha kuwa meneja wake 2014.

Related Posts:

  • Hit Song:Watabamba - Jimmy flavour ft Blacqboi beats Jimmy Flavour ni mmoja ya wasanii toka mkoani Morogoro. amefanya nyimbo kadhaa na zikafanya powa sana ndani ya Morogoro. nyimbo kama Zohari,usingoje nikifa, na kushirikishwa nyimbo kadhaa na msanii Agatha Mbale. Lakini … Read More
  • VIDEO | Agatha Mbale - Wape Habari Mwanamuziki wa Hip Hop toka mji kasoro Bahari Morogoro, Agatha Mbale ametuletea video ya wimbo wake mpya unaitwa Wape Habari, Huu hapa tumekuwekea                … Read More
  • New Audio: Baba wa Taifa - Zombie ft Bestiny Tanzania Tukiwa tunaadhimisha miaka ishirini ya kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa Rais wa kwanza wa Tanzania Mwl. Julius Kambarage Nyerere Baba wa Taifa. Mwanamuziki toka mkoani Morogoro Zombie ametuletea wimbo maalum … Read More
  • Video: Rajram - Pop Corn Official Video ya mwanamuziki mkali wa Free Style kutokea mkoani Morogoro Rajram    (RAJRHYMES )  imekamilika na nipo hewani nkwa ajili yako shabiki na mdau wake .        DOW… Read More
  • New Audio: Roma ft One Six - Anaitwa ROMA Mlisema maeacha, sasa ameanza upyaaaaaaaaa. Ni wimbo mpya kabisa wa ROMA unaitwa Anaitwa Roma akimshirikisha mwanamuaziki ONE 6. Listen to Roma_ft_one_six_anaitwa_roma- Machaku Media byAhmadi Machaku on hearthis.at … Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE