January 22, 2016


Tume ya Uchaguzi ya zanzibar ZEC imetangaza tarehe rasmi ya kurudiwa kwa uchaguzi  mkuu visiwani humo kuwa ni 
2o March 2016 Taarifa hiyo imetolewa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar imebainisha kuwa wagombea wote walioteuliwa hapo awali ndio watakao kuwa wagombea katika uchaguzi huo.
Vile vile Uchaguzi huo utahusisha uchaguzi wa Rais, wajumbe wa baraza la wawakilishi na madiwani na hakutakuwa na uteuzi mpya wa wagombea wala mikutano ya kampeni.
Aidha Chama cha Wananchi (CUF) kimekuwa kikipinga kurudiwa kwa uchaguzi. Chama hicho mapema mwezi huu kilionya kwamba hatua hiyo inaweza kusababisha vurugu, huku chama cha Mapinduzi kikiwataka wanachama wake kujipanga kwa uchaguzi

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE