January 18, 2016

Mkali wa Bongo Flava anaeuwakilisha vizuri mkoa wa Mwanza, Barakah Da Prince, amemtangaza mtayarishaji wa muziki wa siku nyingi kutoka Am records, Bob Manecky  kuwa ndiye mtayarishaji rasmi wa kazi zake za muziki.

Akizungumza juzi na Lil Ommy Barakah ameweka bayana kuwa hata wasanii wengine wakitaka kumshirikisha kwenye nyimbo zao basi lazima Manecky auhusike kwenye utayarishaji.

“Tena naomba niweke wazi kama Manecky ndiye Official Producer wangu, hata nikishirikishwa lazima Manecky aweke mkono wake” Alifunguka Barakah.

Katika ‘line’ nyingine msanii huyo ambaye anatajwa kutoka kimapenzi na muigizaji Nisha, amesema kuwa wiki hii wanasafiri pamoja na Manecky kuelekea jijini Nairobi kwa ajili ya kwenda kukamilisha kolabo kati yake na kundi la Sauti Soul.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE