
Filamu ya The Revenant inaongoza kwa kushindania tuzo vitengo vingi
Waigizaji na waelekezi wa filamu
watakaopigania tuzo kuu za sanaa duniani za Oscar wametangazwa na kwa
mwaka wa pili hakuna watu weusi walioteuliwa.
Filamu ya The
Revenant inaongoza kwa kuteuliwa kupigania tuzo nyingi kwenye tuzo hizo
za 2016, ikiwa kwenye vitengo 12, huku Mad Max: Fury Road ikipigania
vitengo 10.Eddie Redmayne, anayetumai kurudia ufanisi wa mwaka 2015, ameteuliwa kushindania tuzo ya mwigizaji bora dhidi ya Leonardo DiCaprio.

Mwigizaji Idris Elba, aliyeteuliwa kupigania tuzo ya Bafta wiki iliyopita kutokana na uigizaji wake katika Beasts of No Nation hakuwa na nafasi.
Will Smith aliyemwigiza Dkt Bennet Omalu katika Concussion na Jason Mitchell aliyemwigiza Eazy E katika Straight Outta Compton pia hawamo.
Badala yake, filamu ya Straight Outta Compton, imependekezwa kwa ubunifu hii ikiwa na maana kwamba waliotunga hadithi hiyo, ambao ni Wazungu, ndio watakaopigania tuzo pekee.
Mwaka jana, kitambulisha mada #Oscarssowhite kilivuma mtandaoni baadaya waigizaji weusi kutoteuliwa kupigania tuzo hizo, na mwaka huu tena kinavuma mtandaoni.
Mtangazaji Chris Rock, ambaye ni mtu mweusi, ndiye pekee atakayewakilisha ulimwengu wa watu weusi katika tuzo za mwaka huu ambazo washindi watatangazwa tarehe 28 Februari.

Watu weusi ni asilimia 2 pekee kati ya jumla ya watu wanaopiga kura, kwa mujibu wa tovuti ya habari za burudani ya Rollingout.

Mwaka 2014, Mkenya Lupita Nyong'o alijishindia tuzo ya Oscar kwa
uigizaji wake katika filamu ya 12 Years a Slave. Ndiye Mkenya wa kwanza
kushinda tuzo hizo.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment