Hivi karibuni kiungo wa kimataifa wa Kenya anayekipiga katika klabu
ya Southampton Victor Wanyama alimtaja mwanamuziki wa kizazi Alikiba
kwamba ndio muimbaji anyemkubali zaidi kutoka nchini Tanzania.
Kenya
imeendelea kuwa moja ya eneo lenye soko kubwa kwa wasanii wa Bongo
Fleva – na hii imeendelea kudhihirika baada ya mshambuliaji wa
Liverpool, raia wa Belgium mwenye asili ya Kenya Divock Origi ameungana
na Wanyama kwa kusema hakuna msanii wa muziki ndani ya mipaka ya Afrika
Mashariki anayemkubali kama muimbaji wa wimbo ‘Lupela’ Alikiba.
“Unajua mama yangu huwa ana CDs za muziki kutoka Kenya sana, napenda ngoma za Alikiba sana kuliko Diamond ama hao wengine,” alisema Origi, akiongea nyumbani kwake huko Merseyside, United Kingdom na mwandishi wa Pulse Kenya.
Alikiba pamoja na kuimba lakini mpenzi mkubwa wa soka akiwa anaishabikia Yanga pamoja na klabu anayochezea Origi – Liverpool.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment